Tuesday, March 6, 2012

Ahadi kakupa nani?

Hujui safari yako
Alopanga Mola wako
Wakujua utokako
Haujui uendako
Usidhani una muda,
Ukaiacha ibada
Eti utasali uzeeni
Aliyekuahidi Nani?


Chorus:
Ahadi kakupa nani
Kuwa utasali kesho,
Au kunako mwakani.
Au eti mwisho mwisho
wa haya maisha yako?
Ajizi yako ni ghali,
Mwenzangu anza kusali!